Rais wa Nigeria aamuru kuondolewa kwa marufuku ya Twitter Baada ya Kuipiga Block Miezi Kadhaa



Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ameamuru kuondolewa kwa marufuku dhidi ya mtandao wa kijamii wa Twitter,ikiwakampuni hiyo ya kubwa ya teknolojia itafikia masharti flani.
Rais Buhari alisema Wanigeria wanaweza kuendelea kutumia mtandao huo kwa ajili ya "biashara na masuala mengine muhimu".

Katika hotuba yake ya kuadhimisha siku kuu ya uhuru wa nchi hiyo,rais alisema kwamba kamati maalum inajadiliana naTwitterkuhusu masuala kadhaa ya usalama wa kitaifa,ushuru wa haki na utatuzi wa mizozo.

Serikali ya Nigeria ilipiga marufuku huduma zaTwittertangu mwezi Juni baada ya mtandao huo wa kijamii kufuta ujumbe wa RaisBuhariwenye utata.

Marufuku hiyo ilikosolowe vikali na mashirika ya kutetea haki za binadamu na wanaharakati wa kutetea uhuru wa vyombo vya habari.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post