Mwijaku, Juma Lokole Wavuana Nguo





Mwijaku na Juma Lokole ni watangazaji maarufu kwenye mitandao ya kijamii ambao hawaivi kwenye chungu kimoja; kila mmoja amekuwa akimvua nguo mwenzake.

Sasa; kwa mujibu wa Juma Lokole, Mwijaku anampenda Diamond Platnumz kutoka moyoni mwake, lakini ana njaa ya umaarufu ndiyo maana amekuwa akimponda kwani alishakutana hadi na mwanasheria wa Diamond na kumweleza waziwazi kwamba anampenda msanii huyo.

Lokole ambaye ni sapota wa Diamond anasema anavyojua si kweli kwamba, Mwijaku anamchukia Diamond kwa sababu kwenye simu yake hakosi nyimbo za Diamond.

Kwa upande wake, Mwijaku ambaye ni sapota wa Harmonize anasema hataki kulinganishwa na Lokole kwa sababu yeye ana familia wakati Lokole hana ndoa sawa na bosi wake, Diamond hivyo hana cha kushindanishwa naye.
Cc; @sifaelpaul



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post