MSEMAJI Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema serikali imeendelea kutoa fedha za miradi mbalimbali ya maendeleo katika jiji la Mwanza lengo ikiwa ni kuboresha zaidi mkoa huo ambao unashika nafasi ya pili kwa kuiingiza nchi mapato nyuma ya Dar es Salaam, ameyasema hayo leo Oktoba 17, 2021 wakati akitoa taarifa ya wiki ya Serikali akiwa jijini Mwanza.
”Mwanza ni Mkoa wa pili nchini kuchangia fedha nyingi katika pato la Taifa, mwaka 2019 makusanyo ya mapato yalikuwa Sh Trilioni 10.2 na hivyo kuchangia Pato la Taifa kwa 7.35% na mwaka 2020 yalikuwa Trilioni 10.9 hivyo kuchangia Pato la Taifa kwa 7.38.8%,” ameeleza Gerson Msigwa, Msemaji Mkuu wa Serikali.
Ametaja moja ya miradi mikubwa jijini humo ni soko kuu la kisasa linaloendelea kujengwa. ”Tunajenga Soko la Kisasa Mjini ambapo zimeshaletwa Sh Bilioni 8, hadi kukamilika utagharimu Bilioni 20.3, zimeletwa Bilioni 4.5 kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la Abiria kwenye uwanja wa Mwanza ambapo ujenzi ukikamilika utagharimu Shilingi Bilioni 13.3”.
Post a Comment