Vokin Kusic (72) ameamua kujenga nyumba yenye magurudumu kwa chini baada ya kuchoshwa na malalamiko ya mkewe ambaye kila kukicha amekuwa akitaka view mpya (kile wanachokiona kwa mbele wakiwa kwenye nyumba yao).
Bwana huyo Kusic mkazi wa eneo la Bosnia akizungumza na shirika la habari la Reuters amesema kuwa magurudumu hayo yanamsaidia kuizungusha nyumba yake hali inayomfanya mkewe kupata nafasi ya kuona vitu vingine ambavyo havioni kutokana na kuzibwa na kuta za nyumba yake.
“Nimechoka na malalamiko yake na ukarabati wa mara kwa mara wa nyumba ya familia yetu na nikasema ningemjengea nyumba inayozunguka ili aweze kuizungusha na kuona vitu jinsi anavyotaka.” Alisema bwana huyo.
Na: @harith_jaha
Post a Comment