Mwanamke Mmoja Aachwa Kwenye Mataa Baada ya Kuleta Marafiki na Ndugu zake 23 Kwenye Mtoko


Mwanamke mmoja nchini China ameachwa kwenye mataa na mwanaume ambaye walikutana kwenye mtoko (date) wa chakula cha usiku. Tovuti ya Daily Mail imeripoti kwamba mwanamke huyo alialikwa na Mr. Liu ambaye walikuwa hawafahamiani kwa ajili ya kupata chakula pia kuzungumza mapenzi, cha ajabu alikuja na ndugu zake 23.

Taarifa zinasema baada ya kufika hotelini, mwanamke huyo alikuwa na rafiki yake mmoja lakini baadaye walifika ndugu zake wengine 23 hivyo kufanya Bill ya chakula na vinywaji kufikia ($3,165) zaidi ya TSh. MILIONI 7. Mr. Liu aligoma kulipa bill hiyo na kuamua kuondoka hotelini hapo huku akiwaacha na butwaa.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post