Mlanguzi mkubwa wa dawa za kulevya Colombia kuhamishiwa Marekani





Colombia imetangaza kuwa mlanguzi mkubwa kabisa wa dawa za kulevya aliyekuwa anasakwa nchini humo atapelekwa Marekani baada ya kukamatwa Jumamosi. Dairo Antonio Usuga, maarufu kama Otoniel, mwenye umri wa miaka 50, alikamatwa porini katika operesheni ya kikosi cha pamoja cha jeshi, jeshi la angani na polisi. 
 
genge kubwa kabisa la uhalifu nchini humo na amekuwa kwa miaka mingi kwenye orodha ya Marekani ya Shirika la Kupambana na Ulanguzi wa Dawa za Kulevya. Walimtuhumu kwa kuingiza Marekani karibu tani 74 za cocaine kati ya mwaka wa 2003 na 2014. 
 
Waziri wa Ulinzi wa Colombia Diego Molano amesema hatua inayofuata kwa maafisa wake ni kufuata amri ya kuhamishiwa Marekani. 
 
Ivan Duque alipongeza kukamatwa kwa mlanguzi huyo wa dawa za kulevya kupitia ujumbe wa televisheni akisema ni pigo kubwa kwa ulanguzi wa dawa za kulevya nchini humo katika karne hii.
 



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post