Polisi nchini Nigeria wanasema maafisa wa usalama wamefanikiwa kuwaokoa karibu mateka 200 waliokuwa wametekwa na watu wenye silaha Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo.
Polisi wanasema watu waliookolewa ni wanaume 187, wakiwemo watoto na wanawake, ambao walikuwa wametekwa katika nyakati tofauti, katika jimbo ma Zamfara.
Watu waliojihami kwa silaha wamekuwa wakitekeleza visa kama hivi, Kaskazini Magharibi na eneo la Kati nchini humo kwa miaka kadhaa sasa, na baada ya kuwateka watu kwenye vijiji wanaomba fedha kabla ya kuwaachilia mateka.
Imeelezwa kuwa, mateka hao walikuwa chini ya watu wenye silaha kwa wiki kadhaa, na walipatikana baada ya msako wa saa kadhaa kwenye msitu katika jimbo la Zamfara na waliachiliwa bila masharti yoyote.
Wiki iliyopita, jeshi nchini humo lilisema kuwa lilifanikiwa watu wenye silaha wapatao 300, lakini wiki hii, watu wengine wenye silaha wapatao 100 waliwauywa watu 14 kwenye jimbo la Zamfara.
Post a Comment