Maskini R Kelly Awekwa Katika Uangalizi Maalumu ili Asijinyonge


Nguli wa muziki wa R&B toka Marekani, R.Kelly ambaye hukumu yake inatarajiwa kusomwa Mei 4 mwaka 2022, huku kukikwa na uwezekano mkubwa wa kuhukumiwa miaka 10 hadi kifungo cha maisha gerezani, staa huyo ameripotiwa kuwekwa kwenye UANGALIZI wa kina endapo ikitokea anataka kujidhuru (Kujiua) kutokana na sababu mbalimbali za makosa yake mapya.

Kwa mujibu wa Chicago Tribune, wakili wake Bw. Steve Greenberg hakueleza kama R.Kelly ameonesha nia yoyote ya kutaka kujidhuru. Hii imetokana na mkali huyo kukutwa na makosa mengine mapya yanayohusiana na kusafirisha watoto wakike wenye umri mdogo kutoka maeneo mbalimbali kwa lengo la kuwanyanyasa kingono.

Hata hivyo, Greenberg amesema Jaji wa kesi nyingine inayomuhusu R.Kelly alitaka kesi ianze kusikilizwa mapema, lakini yeye na wakili mwingine wa kesi hiyo ya R.Kelly wameomba tarehe nyingine kutokana na wanasimamia kesi za watu wengine. Jaji ameamuru kesi hiyo ianze kusikilizwa Agosti 1 mwakani



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post