JUU ya kusambaa kwa picha wakidaiwa kufunga ndoa, msanii wa Bongo Fleva, Salmin Issa almaarufu Kusah anasema; “Itoshe kusema nimemuoa Aunt!”
Akizungumza na Gazeti la IJUMAA katika pati ya kumbukumbu ya kuzaliwa ya mwigizaji wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel iliyofanyika nyumbani kwao, Tegeta jijini Dar, usiku wa kuamkia jana, Alhamisi Oktoba 28, 2021, Kusah anasema kuwa, watu waelewe hivyo kwamba
mwanamama huyo ni mkewe rasmi.
Kusah ambaye ameachia wimbo wake mpya jana wa I Wish anasema kuwa, akipewa nafasi ya kumzungumzia Aunt ambaye ni mzazi mwenzake, hawezi kumaliza kwani kwa muda mfupi tu wamepitia vitu vingi wakiwa pamoja.
“Aunt amenipa vitu ambavyo siwezi kuvirejesha hivyo itoshe kusema nimemuoa Aunt na ninampenda sana,” anasema Kusah.Kuhusu kupishana kwao umri, Aunt anayesemekana ni mkubwa kwa jamaa huyo, ameibua mjadala mwingine baada ya kudai yeye ana umri wa miaka 28 huku Kusah akiwa na umri wa miaka 29.
Aunt ambaye kwa sasa amebadili dini akitumia jina la Rahma, yeye na Kusah walianza kuwa wapenzi baada ya Aunt kutengana na mzazi mwenzake mwingine ambaye ni dansa wa msanii Diamond Platnumz, Moze Iyobo huku Kusah akiwa ametengana na mzazi mwenzake ambaye ni msanii wa Bongo Fleva, manamama Ruby.
Post a Comment