Kujifungua Kawaida Kwamuogopesha VERA Sidika "Bora Nipigwe Kisu"




SOSHOLAITI maarufu Afrika Mashariki Vera Sidika kutoka nchi jirani ya Kenya amesisitiza kwamba atajifungua kwa njia ya upasuaji na siyo kwa njia ya kawaida kwa sababu anaogopa uchungu wa leba.


Vera ambaye anatarajia kujifungua muda wowote anasema kwamba, alifanya uamuzi kuwa atajifungua kwa njia ya upasuaji hata kabla hajapata ujauzito.


Vera ambaye anatarajia mtoto wake wa kwanza ameapa kwamba hakuna yeyote ambaye anaweza kubadilisha uamuzi wake.


Mpenzi huyo wa mwanamuziki Brown Mauzo amesema kwamba ni heri avumilie kipindi cha uponyaji baada ya kufanyiwa upasuaji kuliko akabiliane na machungu ya leba.



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post