Kiongozi wa kijeshi nchini Guinea Kanali Mamady Doumbouya ameapishwa kuwa Rais wa mpito baada ya kuondolewa kwa Alpha Condé.
Kiongozi huyu wa jeshi mwenye umri wa miaka , 41, anakuwa kiongozi wa pili mdogo barani Afrika ,akifuatiwa na rais wa Mali, Assimi Goïta,mwenye umri wa miaka 38, ambaye pia aliongoza mapinduzi ya kumuondoa Rais Keita.
Anatarajiwa kuunda serikali katika wiki chache zijazo.
Baada ya mapinduzi ya Guinea Kanali Doumbouya alisema askari wake wamechukua uongozi na walitaka kumaliza ufisadi, ukiukwaji wa haki za binadamu na usimamizi mbaya uliokithiri nchini humo.
Rais Condé alichaguliwa katika uchaguzi uliokumbwa na utata kuongoza kwa muhula wa tatu licha ya maandamano ya ghasia mwaka jana.
Umoja wa Afrika na Ecowas wameiwekea vizuizi Guinea, wakilitaka taifa hilo lifuate katiba ndani ya miezi sita.
Post a Comment