Kibaka Amchoma Kisu Askari na Kumuibia



 

JESHI la Polisi nchini Kenya wanamsaka kijana mmoja kibaka ambaye alimvamia na kumjeruhi ofisa wa polisi wa mwanamke katika eneo la Ngomongo jijini Nairobi kisha kumshambulia vibaya kabla ya kumuibia na kutokomea na vitu vya askari huyo.

Kisa hiho kimetokea Jumapili iliyopita, Oktoba 17 ambapo askari huyo wa kike anayekuwa akilinda katika Jengo la Kimataifa la Mikutano la Kenyatta (KICC), alikuwa akielekea nyumbani kwake wakati alipovamiwa na kibaka huyo.

Kulingana na ripoti ya Polisi, mwizi huyo asiyejulikana alimdunga afisa huyo kisu mgongoni na kumuibia vitu vyake alizokuwa nazo. Afisa huyo alipata majeraha mabaya na kukimbizwa hospitalini ambapo kwa sasa anaendelea kupata nafuu.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post