Inachekesha..Wamarekani Hawamfahamu Diamond, Wazani ni Mchezaji Mpya wa Timu yao


Baada ya Timu ya @washingtonnfl kumzawadia Jezi na kumpost @diamondplatnumz kwenye page yao ya Instagram, mashabiki wa timu hiyo wameonekana kushangazwa na mtu huyu, huku wengi wakijua ni mchezaji mpya wa timu yao.

Maswali mengi yameibuka kutoka kwa mashabiki hao mfano "Who?", "Who is that?" "Can he play" "Can he Help our Team", "Serious Question who is this" Baadhi ya wabongo na waafrika wameonekana kujibu baadhi ya comments za wamarekani kwa kusema kwamba huyu ni msanii kutoka Afrika, East Africa na Wengine wakaitaja Tanzania.

Kumbe wasanii wetu Usikute Show zao za marekani huwa wanahudhuria wabongo tu labda na wakenya wa huko, maana hili jambo limeonesha wazi kuwa wasanii kutoka Tanzania hawafahamiki, yani wanajua mchezaji mpya kasajiliwa


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post