-Wanaojua kuzungumza Kiingereza hata kama wanazungumza Kiingereza "broken". Wote ni mashahidi, hawa Siku zote hujihisi wao ni bora na maisha wameyapatia.
- Wanaomiliki matoleo mbalimbali ya simu za iPhone. Siongezi neno kuhusu kundi hili.
- Waliochukua mkondo wa masomo ya sayansi walipokuwa sekondari na baadaye wakaenda vyuo vikuu kusomea kozi mbalimbali za uhandisi. Hawa hata ukiwakuta mtaani bila ajira, wanajihisi tayari wameyapatia maisha.
- Wahitimu vijana wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Siongezi neno kuhusu kundi hili.
- Vijana wa Kitanzania ambao kwa wakati fulani waliwahi kuishi Marekani au Uingereza harafu kwa sasa wamerudi Bongo kupambana na msoto wa maisha.
- Wanaomiliki gari jamii ya Vitz, IST na Altezza. Jeuri na mikwara yao barabarani inatupa picha halisi.
- Wanajeshi vijana miezi yao kwanza kwenye ajira Jeshini harafu uwakute Uraiani wamevaa zile sare zao zenye mabaka mabaka.
Ongezea wengine unaowajua.
Karibuni.
Post a Comment