Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kuwa kuna watumiaji wa mitandao ya kijamii Bilioni 4.2 duniani ambao ni zaidi ya asilimia 53 ya idadi ya watu ulimwenguni kote.
Mtandao wa Facebook ndio unaongoza kuwa na watumiaji wengi wakifikia zaidi ya Bilioni 2.7, licha ya umaarufu wa Instagram, ina watumiaji Bilioni 1.2 tu na kushika nafasi ya tano.
Hii ni orodha ya wasanii wa Bongofleva ambao wanaongoza kwa Likes (followers) kwenye mtandao wa Facebook.
1. Diamond Platnumz - Milioni 6.6
2. Harmonize - Milioni 3.0
3. Alikiba - Milioni 2.5
4. Zuchu - Milioni 1.29
5. Nandy - Milioni 2.12
6. Rayvanny - Milioni 2.11
7. Lady Jaydee - Milioni 1.8
8. Lava Lava 1.6
9. Marioo - Milioni 1.4
10. Queen Darleen 1.3
11. Vanessa Mdee - Milioni 1.0
12. Mwana FA - 919K
13. Rich Mavoko - 830K
14. AY - 787K
15. Rosa Ree - 746k
Post a Comment