Licha ya jitihada za kujenga himaya yake katika muziki huo, Harmonize ameonekana kuwa msanii wa 'kukopi na kopesti' mambo mengi katika muziki wake jambo ambalo linaacha maswali mengi Sana.
1. JINA LA JESHI, TEMBO : Kwa kipindi kirefu amekuwa akitumia majina ya Jeshi na Tembo, lakini ukweli tayari majina hayo kuna wasanii walishaanza kuyatumia kabla yake na bado wapo kwenye muziki.
Kundi la Navy Kenzo ndio wakwanza kutumia jina la Jeshi na ni asili yake ni neno, 'Navy' ambalo ni sehemu ya jina la kundi hilo.
Jina la Tembo lilinza kutumika na Alikiba toka mwaka 2015 pale alipochaguliwa kuwa balozi kwenye kampeni iliyosimamiwa na serikali na shirika la kimataifa la WildAid iliyolenga kukomesha ujangilili wa tembo.
2. ALBAMU YA AFRO EAST, A BOY FROM TANDALE : Inavyoonekana Albamu yake ya kwanza, Afro East imeiga vitu vingi kutoka kwenye albamu ya Diamond, A Boy From Tandale kama ifuatavyo;
Mosi; tarehe, Machi 14, 2018, Diamond alizindua albamu yake Nairobi nchini Kenya, naye Harmonize akazindua yake Machi 14, 2020 Mlimani City, Dar es Salaam.
Pili; albamu hizo mbili zina idada sawa ya nyimbo, yaani zote zina ngoma zipatazo 18.
Tatu; A Boy From Tandale imemshirikisha msanii mmoja pekee wa kike kutokea Tanzania ambaye ni Vanessa Mdee aliyesikika kwenye wimbo uitwao Far Away, hivyo hivyo Afro East ikimchukua Lady Jaydee aliyesikika kwenye wimbo uitwao Wife.
3. WIMBO PAPA WEMBA, ROSA REE : Agosti mwaka jana Rosa Ree alimshtaki Harmonize kuchukua mdundo wa wimbo wake 'Kanyor Aleng' bila idhini yake na kuutumia katika wimbo wake uitwao Ameen jambo hilo likapelea wimbo huo kufutwa YouTube kwa kukiuka taratibu za hakimiliki.
Huo ulikuwa ni wimbo wa pili kwa Harmonize kuondolewa YouTube, wa kwanza ni Uno ambao Prodyuza wa Kenya, Magix Enga alipeleka malalamiko yake kwenye mtandao huo.
Pia albamu yake, Afro East iliwahi kufutwa kwenye mitandao kama Tidal, Amazon, Deezer, Yandex na YouTube Music kutokana na wimbo 'Your Body' ambao amemshirikisha Burna Boy kutokea Nigeria kuchukua vionjo kutoka kwenye wimbo wa Marehemu Papa Wemba uitwao Show me the Way, hiyo ni kutokana na kile inachodai hakuzingatia taratibu za hakimiliki.
Post a Comment