Hamisa Mobetto Atahadharishwa Ukaribu Wake na RICK Ross "Utaachiwa Watoto Ulee Mwenyewe"




WIKI kadhaa baada ya rapa wa kiwango cha dunia, Rick Ross kukiri kwamba ana koneksheni na mwanamitindo Hamisa Mobeto wa Tanzania, ametapata majanga.

Kwa mujibu wa nyaraka za kisheria zilizovuja kwa wadaku nchini Marekani, Rick Ross anatakiwa kulipa Dola za Kimarekani elfu 11 (zaidi ya shilingi milioni 25 za Kitanzania) kwa mwezi kwa mwanamke aitwaye Briana Singleton kwa ajili ya matunzo ya watoto watatu aliowatelekeza.

Dokyumenti hizo zinamtaka Rick Ross, mbali na kiasi hicho cha pesa pia anatakiwa kulipa bima za afya na mambo mengine ambayo jumla yake ni shilingi milioni 15 kwa mwezi.


Baada ya kusambaa kwa taarifa hizo, baadhi ya mashabiki wamemtahadharisha Mobeto kuwa makini na jamaa huyo la sivyo naye ataachiwa watoto alee mwenyewe.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post