Cristian Ronaldo alipitia maisha ya kimasikini akiwa mdogo alimwambia baba yake kuwa watakuwa matajiri watakuwa na nyumba kubwa. Christian Ronaldo pamoja na vikwazo vyao alikuwa na imani kubwa aliamini siku yake inakuja aliendelea kupambania ndoto zake.
Lakini baba yake kwa kuzingatia hali halisi jinsi ilivyongumu kuvunja minyororo ya umasikini alimwambia mwanangu hilo haliwezekani . Hakuwa na imani kuna siku watatupa minyororo ya umasikini na kuishi maisha mazuri nyumba kubwa nk.
Leo Familia yake imekuwa maarufu na tajiri kupitia Christian Ronaldo aliyejitoa kikamilifu kubadili historia ya nyumbani. Leo maneno aliyomwambia baba yake akiwa mdogo yametimia lakini baba yake hayupo amelala mauti.
Ikiwa unapambana pambana amini katika ndoto zako kukosa imani ndio kunawafanya watu wasiweze kupambania ndoto zao kikamilifu na kuvishinda vikwazo. inawezekana na sisi kufanikiwa kama tunaimani kama tuna pambana kweli kweli kama tuna nidhamu kwenye kila kitu.
Mohamed Ali anatukumbusha kuwa”Haiwezekani ni neno lililosambazwa na watu wachache walioridhika na namna wanavyoishi ,bila kutambua uwezo walionao kuibadilisha dunia wanayoishi”
UNAONA MUDA UMEKUACHA LAKINI KAMWE USIIKATIE TAMAA NDOTO YAKO IPAMBANIE HADI IWE YAKO
Post a Comment