Habari za Hanstone Hawa Wao WCB Hawaelewi Kinachoendelea, Mkubwa Fella Afunguka

 


Moja ya stori kubwa kwenye mitandao ya kijamii hapa bongo ni ishu ya msanii Hanstone ambaye inasemekana alisainiwa WCB na ameamua kujitoa baada ya kusugulishwa benchi kwa muda mrefu. Hili limekuja baada ya kuachia EP yake kwa mara ya kwanza (YouTube) kisha akaifuta kabla ya kuirejesha tena kwa mara ya pili lakini cha ajabu haina Logo za Label ya Wasafi.

Hasa kwenye Vimbweta vya umbea (U-HEARD), Desa boy @soudybrown amewavutia waya Hanstone mwenyewe, @mkubwafellatmk pamoja na @ricardomomo ili kujua undani wa suala hili. Kwa Hanstone amedai hayuko tayari kuliongelea kwasasa sakata hilo na akakata simu.

Alipotafutwa Ricardo Momo amedai ishu za Hanstone kiukweli hazijui maana kwasasa hayuko kabisa kwenye hiyo michongo. Labda wangetafutwa mameneja kama Tale au Fella wangeweza kulitolea ufafanuzi vizuri.

Kwa upande wa Mkubwa Fella amedai hayuko kwa watoto huko (hasimamii wengine zaidi ya Diamond) lakini hata kama Hanstone angekuwa amesainiwa WCB basi watu wangejua,maana katoa kazi ambazo hazina hata Logo ya Label hiyo kitu ambacho si rahisi kwa msanii ambaye yupo WCB akiishia kusema kiukweli halijui hilo suala labda atafutwe msanii mwenyewe. ( “Soudy eeh,sijui rafiki yangu wala sidanganyi ingekuwa kweli ningekwambia).



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post