Ugomvi wa Alikiba na Shilole umeonekana kuendelea kupita na wengi,na raundi hii umehamia kwa Barakah the Prince na Gigy Money,hii imetokana na insta live ya Gigy Money baada ya kumwambia Alikiba kipaji bila nidhamu atakuwa kama Barakah.
Barakah ametumia ukurasa wake wa Instagram kumchana Gigy Money kwa alichokifanya, huku akitumia kauli nyingi za dharau na kuambatanisha picha zake za nusu utupu. Kwa upande wa Gigy Money amecomment na kumuahidi Barakah kuwa atamtolea mafile yake maana anamjua nje ndani.
Post a Comment