Kupitia ukurasa wake wa Twitter Kamwaga amesema watu wengi wamekuwa wakimtupia lawama Samatta pindi timu inapofanya vibaya tu lakini inapofanya vizuri wanawapa sifa watu wengine.
✍“Utusamehe sisi Watanzania kwa kukubebesha mzigo mzito. Kila timu ikifanya vibaya, zigo la lawama lote kwako. Ikifanya vizuri, sifa kwa wengine” ameandika Kamwaga katika ukurasa wake wa Twitter.
Kamwaga ameandika ✍“Wakati wa kukusifu na kuimba jina lako utafika. Ulitupeleka AFCON na sasa kuna ndoto nyingine kubwa zaidi. Ahsante sana” amesema Kamwaga.
Taifa Stars jana ilishinda bao 1-0 dhidi ya Benin katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia nchini Qatar 2022.
Post a Comment