Mtangazaji tokea Wasafi Fm, Diva the bawse amedai amewahi lipwa milioni 5 na msanii mkubwa kwenye ramani ya muziki (bila kumtaja jina) ili tu aigize nae mahusiano,lengo likiwa ni kumboost arudi kwenye game kama zamani na pesa ilipokata na mkataba ukamalizika.
“Confession: Mimi Kama Diva Nakiri Nililipwa Milioni 5 • Niigize Mahusiano na mtu ili Kum boost Na Kumrudisha Msanii Huyo Mkubwa tu Tanzania katika Ramani Ya Muziki .. alirud kwa nguvu zote ila Mkataba wangu wa maigizo ulipoisha ambapo ilibidi tuachane hela ishaisha apo Watanzania bila kujua wali mind couple yetu kuvunjika!.”- Diva
Wengi wanamuhusisha Alikiba, lakini Alikiba alirudi kwenye game 2014 kipindi ambacho Diva hana fame hiyo ya kumbabaisha mtu na hakuna mtu alimind maana haikuwahi kujulikana kama hao watu wanadate.
Kuna wanaomuhusisha memba wa kundi la zamani la muziki wa Bongo Flava la East Coast Team, King Crazy GK,alirudi kwenye game 2017/2018 kipindi Diva ana fame,ila nani alimind uhusiano huu?😁 na iko wazi walikuwa wanadate serious.
HABARI KAMA HIZI DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL KWA KUBONYEZA HAPA
Au Kheri Music? Hiyo milioni 5 ya mkataba alitoa wapi? Kwanza hajawahi kuwa msanii mkubwa hapa bongo wala kupotea na kurudi.
Post a Comment