Dizaini kama msanii @diamondplatnumz hataki kuchukuliwa kawaida kwenye gharama ya viwalo anavyotupia lakini pia sehemu ya wapi viwalo vyake vinatokea, na hii ndio imefanya amkwepe muuza viwalo maarufu Dar es salaam, @chiddimapenzi ambae alipost moja ya picha ambayo inamuonyesha Diamond akifanya Sound Check kuelekea shoo yake ya Minnesota tarehe 15 mwezi huu, na kuiandikia Caption kumshukuru msanii huyo kwa support aliyompa.
Kitendo hicho kimemfanya Diamond acomment kwenye post hiyo akimuuliza support gani anayoizungumzia kwenye hiyo picha. Chid ameifuta post hiyo na kupost tena akibadilisha Caption kuwa pamba alizopigilia Diamond zinapatika Dukani kwake Kinondoni huku akimsalute tena kwa support.
Wapo wanaochukulia kama Chid anasaka Kiki huku baadhi wakidai ni kweli Mondy alidondoka Dukani kwa Chid kujipatia ming'ao ya kupigilia U.S A. Lakini @chiddimapenzi mwenyewe amethibitisha vile viwalo vya Mondy vimetoka dukani kwake na wamefanya kazi na msanii huyo kwa takribani miaka 10. Mbali na hilo pia Diamond hii leo,tarehe 13 amenunua saa yenye gharama ya zaidi ya milioni 60 za kitanzania.
Post a Comment