Burna Boy Atamani Kuwa Kama Dada Yake




Mshindi wa Tuzo za Grammy na mwanamuziki kutoka Nigeria, Burna Boy ameonesha kufurahishwa na hatua ya dada yake Nissi ya kuwa sehemu ya waundaji wa toleo jipya la gari la Range Rover lililozinduliwa hivi karibuni.

 

Nissi katika ukurasa wake wa Twitter  alipost picha za gari hilo huku akiambatanisha na ‘caption’ iliyosomeka: ‘’After 3 years working on this project I’m proud and happy to see it now revealed to the world’’ (Baada ya miaka mitatu ya kuufanyia kazi huu mradi, sasa najivunia na nina furaha kuuona umeingia sokoni).

 

Kaka wa dada huyo ambaye ni Burna Boy, Oktoba 28 katika ukurasa wake wa Twitter naye alionesha kufurahishwa mno na hatua kubwa aliyoifikia dada yake, Burna Boy aliandika: ‘’I  want to be like you when i grow up @NissiNation)’’ (Nikiwa mkubwa , natamani kuwa kama wewe Sissi).

Tuambie unajivunia nini kwa dada uliyenaye!




0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post