Idris Okuneye, ni mmoja wa watu maarufu Nigeria umaarufu uliojengwa zaidi na taarifa zake mitandaoni. Idris anayefahamika zaidi kwa jina la Bobrisky, anasema wanawake wameshindwa kutumia vizuri kile Mungu amewapa
Bobrisky amesema hayo katika kipindi cha mahojiano cha Televisheni Chude #WithChude.
Haya ni mahojiano ya kwanza aliyoyafanya Bobrisky na kuonekana kwenye Televisheni kwa mwaka huu wa 2021 mwaka ambao anasheherekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwake miaka 30 iliyopita.
Linapokuja suala la "ulizaliwa mwanaume, kwanini unataka kujibadilisha na kuwa mwanamke", anasema Bobrisky:
"Kwa sababu kuwa mwanamke kwa sasa imefungua fursa nyingi. Wanawake hawajui kwa namna gani wana nguvu, wengi wao hawajui kutumia vipaji vyao kama wanawake."
Alisema wakati akiwa mwanaume hajabadilisha jinsia, hakuwa na pesa, na hakuna aliyeshughulika naye kwa sababu hakuwa na pesa. "Nilikuwa napambana".
Bobrisky akaamua kwamba hataki hali hiyo , alitaka kuwa mtu anayejisimamia mwenyewe.
Bobrisky
Chanzo cha picha, Bobrisky/Facebook
"Hata hivyo," anasema Bobrisky, "wapo wasiojali hilo."
Idris alikuwa karibu na mama yake kabla hajafariki. "Ni mtu pekee aliyenipenda sana na kuniunga mkono wakati kila mmoja alikuwa akinikataa."
"Pesa ni kila kitu. Kama unasema pesa sio kila kitu, unajidanganya mwenyewe. Unahitaji kuwa na hadhi fulani, ikiwemo pesa.
Kwa namna gani Bobrisky amejibadili na kuwa mwanamke?
Maisha ya Bobrisky yako mtandaoni sasa, na amekuwa akikataa kuzungumza hali yake ya sasa.
Anachosisitiza ni kwamba anataka kujisimamia mambo yake mwenyewe, akitaka kutumia alichonacho kupata anachotaka bila kujali akina nani wanasema nini , anasema waseme wanavyotaka hajali.
Julai 8, 2021 alionesha umma mwili wake mpya baada ya kufanyiwa upasuaji ili aonekane mwanamke zaidi. Ingawa muonekano wake ulianza kuonekana hivyo kwa miaka kadhaa huko nyuma.
Mei 2019 alijitokeza hadharani kwa mara ya kwanza na kusema anataka atambulike kama mwanamke na sio mwanaume.
Hatua hiyo ilipokelewa kwa hisia tofauti hasa kwenye mitandao ya kijamii. Alipokea ujumbe mwingi wa dhihaka kwenye ukurasa wake wa instagram
Kwa muda mrefu Bobrisky amekuwa akikumbana na maneno makali ya kupinga hatua yake ya kujibadili kutoka mwanaume kuwa mwanamke.
Wapo wengi wanaomuona kama mtu aliye na matatizo kwa uamuzi huo, kulingana na mila na tamaduni za Kiafrika, lakini wapo pia wanaoona uhuru wake wa kimaamuzi unapaswa kulindwa.
Mwaka 2016 Meneja wa mawasiliano wa Google Afrika Magharibi, alisema Bobrisky alikua anaongoza kama mtu aliyesomwa na kutafutwa sana habari zake kupitia Google nchini Nigeria.
Umaarufu wake umemfanya kutumika kwenye shughuli mbalimbali za kijamii zikiwahusisha pia watu maarufu wakiwemo waigizaji.
Post a Comment