AZAM FC ikiwa uwanja wa nyumbani wa Azam Complex, Dar, jana ilikubali kubanwa na wageni
wao, Pyramids katika mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika.
Mchezo huo wa hatua ya kwanza uliomalizika kwa timu hizo kushindwa kufungana, timu zote zilionekana
kucheza kwa kasi ya chini ambayo ilikuwa faida kwa wageni walioonekana mapema kwamba wamekuja kutafuta sare.
Baada ya mchezo huo, Kocha Msaidizi wa Azam FC, Vivier Bahati, alisema haikuwa bahati kwao kupata ushindi, lakini wanajipanga kufanya vizuri ugenini.
“Nyumbani tumeshindwa kupata ushindi, tulipata nafasi ambazo tulishindwa kuzitumia vema, hivyo tutaiandaa timu kuona tunafanya vizuri ugenini,” alisema Bahati.
Timu hizo zinatarajiwa kurudiana wikiendi ijayo nchini Misri ambapo mshindi wa jumla ataenda kucheza mechi
za mtoano kusaka nafasi ya kutinga.
Post a Comment