MWANAMKE anayemshutumu Cristiano Ronaldo akidai mwanasoka huyo alimbaka, ametaka alipwe fidia ya Pauni milioni 56 (zaidi ya Sh bil. 170 za Tanzania).
Katika nyaraka mpya za mahakama, bibiye Kathryn Mayorga ambaye ni mwanamitindo wa zamani, anataka apewe mkwanja huo kwa unyama aliodai kufanyiwa mwaka 2005.
Katika kesi ya msingi, Ronaldo anadaiwa kumbaka Kathryn aliyekuwa na umri wa miaka 25 wakati huo, tukio lililotokea katika moja ya hoteli za jijini Las Vegas, Marekani.
Hata hivyo, mara zote Ronaldo anayekipiga Manchester United akiwa pia ni nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amekuwa akikanusha kuhusika katika unyama huo.
Post a Comment