Karibu watu 4,500 wameugua kusini mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kufuatia kuvuja kwa sumu kutoka kwa mgodi wa almasi katika nchi jirani ya Angola, waziri wa mazingira anasema.
Eve Bazaiba alisema watu 12 walikuwa wamefariki dunia. Alisema kuwa DR Congo itauliza fidia ya uharibifu uliosababishwa lakini haikutaja kiasi.
Hata hivyo, hadi kufikia hivi sasa hakuna aliyesema chochote kujibu hayo hasa kutoka kwa kampuni ya madini.
Mwezi uliopita kulikuwa na uvujaji wa kutoka eneo la uhifadhi wa bidhaa za vyuma vizito uliosababisha mto kuwa na rangi nyekundu, samaki, viboko na wanyama wengine wakafa.
Credit by BBC.
Post a Comment