Dodoma. Serikali ya Tanzania imewaonya wanaume wenye umri mkubwa kuachana na tabia ya kujihusisha na mapenzi na wasichana wadogo.
Kauli hiyo imetolewa leo Alhamisi Septemba 8, 2021 na naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia wenye ulemavu, Ummy Ndeliananga wakati akifungua mkutano wa vijana wanaoishi na virusi vya ukimwi.
Amesema vijana wadogo wa kike kuwa na mahusiano ya kingono na wanaume wenye umri mkubwa kwa kuvutika na vishawishi kama pesa na zawadi ndogo ndogo.
“Kwa mara nyingine tena natoa rai kwa wanaume wenye umri mkubwa kuachana na tabia ya kujihusisha na mapenzi na wasichana wadogo,”amesema.
Amesema Serikali haitasita kuchukua hatua kali za kisheria kwa yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo hivyo.
Aidha, Ummy amesema takwimu zinaonesha kuwa vijana wengi wanaojihusisha na mapenzi hawatumii kinga na wengine hutumia mara moja tu na baada ya kuzoeana huendelea na mahusiano ya ngono bila kinga yoyote.
Mwenyekiti wa Baraza la Watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (Nacopha), Leticia Kapela amesema pamoja na jitihada hizo, bado kuna changamato zinazoendelea kujitokeza siku hadi siku.
Post a Comment