WATU watatu waliokuwa wamebebana kwenye pikipiki (Mshikaki) wamefariki dunia papo hapo baada ya kugongwa na fuso lenye namba za usajili T507 BCF majira ya saa 12 jioni katika eneo la Tazegwa katika barabara itokayo Nzega Mjini kuelekea Tabora.
Kamanda wa Polisi mkoani Tabora Safia Jongo, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 9, amesema vijana hao wenyeumri wa miaka 15 hadi 18 amesema ajali hiyo ilitokea Septemba 7, mwaka huu, na kwamba pikipiki waliokuwa wamebebana marehemu hao haikuwa na namba ya usajili.
Aidha, Jongo amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni madereva wa pikipiki walikuwa wanatoka Nzega Mjini na kuelekea katika kitongoji cha Shagiro na walipofika eneo hilo la Tazegwa walizi-overtake gari mbili aina ya malori pasipo kuangalia vizuri na ndipo walipokutana uso kwa uso na fuso na kugogwa na kupoteza maisha pale pale.
Hata hivyo Kamanda huyo ameendelea kusema kuwa vijana hao watatu waliokuwa katika pikipiki hiyo moja walikuwa katika mwendo wa kasi na ajali hiyo imetokana na kutokuwa na umakini pindi wanapokuwa barabarani.
Kamanda Jongo amewataja walifariki katika ajali hiyo kuwa ni Paulo Petro,Rubeni Jogi na mwingine alitambulika kwa jina moja la Nasoro.
Post a Comment