Vita Nzito ya Ma-Baby Mama wa Mondi





AMKENI…amkeni… kumekucha! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya kuibuka kwa vita nzito baina ya wazazi wenza (ma-baby mama) wa staa wa muziki nchini Tanzania, Diamond Platnumz ambao ni Zari The Boss Lady, Hamisa Mobeto na Tanasha Donna, IJUMAA WIKIENDA limesheheni ubuyu kama wote.

 

Inafahamika kwamba, Zari amezaa watoto wawili na Diamond au Mondi ambao ni Tiffah Dangote na Prince Nillan wakati Hamisa amezaa naye mtoto mmoja wa kiume aitwaye Dyllan na Tanasha naye amezaa naye mtoto mmoja wa kiume ambaye ni Naseeb Junior au NJ.

 

Sasa; baada ya Hamisa na Tanasha kudaiwa kufanya upasuaji au sajari kwa ajili ya kuongeza kalio na kutengeneza shepu matata namba nane, timu zao zimeendelea kumshambulia Zari kwamba amefunikwa na wenzake hao hivyo kupoteza mvuto mbele ya Mondi au Simba wa Tandale.



Watatu hao; wote wanatajwa kufanya upasuaji kwa kuwa shepu walizonazo sasa siyo walizokuwa nazo mwanzoni.

Katika vita kali inayoendelea mitandaoni, timu ya Hamisa (Team Hamisa) imeungana na ile ya Tanasha (Team Tanasha) ambapo kwa pamoja zinaishambulia ile timu korofi ya Zari (Team Zari).

 

“Acheni kuharibia watu siku. Hamisa hashikiki. Mrembo sana. Hapa Uingereza tunajua urembo. Hamisa ni mrembo kupita kiasi, tena mnamfananisha Hamisa na Tanasha kwa Zari? Zari ni kama mama yao, mwambie akubali umri umekimbia ila simchukii yeyote…”

 

“Tanasha ni moto wa kuotea mbali. Zari amezeeka, hafai kulinganishwa na watoto wadogo…”

“Zari Zari Zari Zari namba moja. Ni mzuri, mpambanaji, mrembo Afrika yote. Hakuna kama Zari…”

“Aulizwe Diamond, yeye ndiye anajua…”

 

“Zari ndo mwenye muonekano wake waasiri Hawa wawili tanasha na mabeto wao wamejiwekea michina tu…”

“Kwa vile mondi ni muislaam na anaruhusiwa kuoa hata wake wanne ni bora angewaoa wote na akamuongeza na wema ingekua poa saana…”

Inasomeka sehemu ya maoni lukuki juu ya mpambano huo.



Katika siku za hivi karibuni, Diamond amekuwa haeleweki yupo upande gani kwani kuna kipindi alikuwa na ukaribu na Zari, lakini uwezekano wa kurudiana ukawa mgumu mno.

 

Hata hivyo, uchunguzi wa gazeti hili umebaini kwamba, awali Hamisa alikuwa haivani na mama mzazi wa Diamond, Mama Dangote, lakini siku za hivi karibuni wanaonekana kumaliza tofauti zao.

 

Lakini kwa upande wa Tanasha, Mama Dangote amekuwa akieleza namna ambavyo alimkubali mno mwanamama huyo hivyo baadhi ya watu kuamini kwamba huwenda wakarudiana.

STORI; MWANDISHI WETU


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post