Jay-Z na timu ya wanasheria wake wanapambana kumsaidia mzee wa miaka 55 ambaye alihukumiwa kifungo cha miaka 20 gerezani kwa makosa ya kusambaza na kukutwa na bangi zaidi ya Tani moja.
Kwa mujibu wa mtandao wa Page Six, mfungwa huyo aitwaye Valon Vailes alimuandikia barua Jay-Z akimtaka amsaidie kuachiwa huru kutokana madai kwamba mahakama haikutenda haki. Jay-Z baada ya kuisoma barua hiyo aliguswa na kumkabidhi mwanasheria wake Alex Spiro kulifanyia kazi.
Post a Comment