Mwana alijifanya mwanamke kipindi hicho katikati ya miaka ya 2000 akaweka profile picha ya mdada aliitoa instagram ni pisi kinyama. Na aka apload picha za huyo mdada kibao.
Sasa wanaume wakawa wanavutiwa sana na mwana.. wanaomba namba mwana ana wapa. Wakipiga anadai mic mbovu wachati. Kwenye whatsapp kaeka picha ya huyohuyo mdada.
Mwana akawa anapewa vocha kibao maana akiombwa picha anadai bundle halitoshi anaungwa la mwezi. Kashatumiwa sana nauli aende mikoani kubanduliwa anachukua then anatafuta sababu za kutokwenda. Mwana akiingia mp anaomba hela kwa wanaume wa badooo anapata.
Anatafuta zile nudes za watu weusi wenye maumbo ya kufanana na ile picha anayotumia halafu anawatumia wakulungwa anaziba sura. Wakulungwa wanapagawa kinoma yani, voice note kibao wAnatuma wAnaomba sauti, mwana anampanga dem wowote wanatuma voice note na maneno ya mapenzi.
Yule dem wa insta akipost picha mwana anaziwah anachukua anazitumia badoo. Mwana kafanya sana ushetani.. wengine walimshtukia kama ni mwana lakini hawakuwa na cha kufanya.. hawajui watampata wapi. Utaenda kushtaki vip police!? Utasema kuna jamaa anajifanya mwanaume badoo anakula hela zetu!? Si watakucheka!? Hahaha hahaha
Mwana akipotea siku mbili hewan akiwasha data anakuta ma message kibao.. mwana anasema simu imeharibika hana hela so anaazima ya rafiki yake mara moja moja kuingia mtandaoni.
Mwana alikuwa full package yaani anacheza sana na akili zao.. kumbuka hapo mwana hana kazi wala nini.. hiyo ndo kazi yake, bonge la scam yaani tapeli balaa.
Mwana kwa week akikusanya hela za wa kulungwa zinafika laki tatu. Mwana akawa conman kinoma. Akawa hana huruma kabisa na wakulungwa wa mitandaoni, alikuwa anasema anawafunza adabu wazee waliioa.
Similar News:
Job Opportunity at Prime Minister’s Office, Procurement Officer
Aliwapasua anavyotaka yeye yaani wanaoshtukia game mapema wanamchana wanamtukana mengi matusi kwa sauti ya ukali lakin haisaidii coz washaliwa pesa zao. Mwana akazoea akaja akaacha huo mchezo maana wengi walimstukia akaamua kustaafu.
Noma sana. Hii ni true story kabisa mm shahidi.
Thebogo055/JF
Post a Comment