MBUNGE wa Buchosa, Eric Shigongo ameiomba Serikali kufanya mapitio ya baadhi ya tarrif za kodi ambazo zimekuwa mwiba kwa wafanyabaishara kuendesha biashara zao hapa nchini.
Shigongo amesema hayo wakati akizungumza Bungeni kuchangia mabadiliko ya sheria mbalimbali na kuongeza kuwa nchi inatakiwa kuwawezesha wafanyabiashara kwa kuwapa mikopo yenye riba nafuu ili kuinua biashara zao na uchumi wa taifa.
“Niliposoma mkataba huu niliingia hofu, nikadhandi mkataba huu utaua viwanda vteyu na kuondoa ajira zetu. Lakini baadaye nikasoma zaidi upande wa pili nikagundua vitu vizuri kwenye mkataba huu unakwenda kuifanya Afrika kufanya biashara yenyewe kwa yenyewe jambo ambalo huko nyuma lilikuwa halifanyiki.
“Nilipofika hapo nikachagua kuunga mkono mkataba huu na kuachana na hofu kwa sababu utakuwa na manufaa kwa Taifa letu.
“Ukitaka kuichelewesha Afrika isababishie kusiwe na ushirikiano, Wakoloni waliweka mipaka ardhini mwetu na mipaka hiyo imehamia vichwani mwetu, hii ndio inachelewesha maendeleo yetu. Tunaogopa kufanya maamuzi. Mkataba huu unaenda kuondoa vizuizi vya kibiashara kati yetu na wenzetu. Tutaanza kufanya biashara kati ya Taifa na Taifa.
“Hapa tunazungumza mahindi lakini ninaamini kuna mataifa hayana mahindi na wanaweza kuagiza mahindi Brazil badala ya kuagiza Tanzania. Tukubali kwenda kujifunza tukiwa tunafanya, tutarekebisha huko ndani kwa ndani hatimaye tutafanya vizuri.
“Jambo la muhimu lazima nchi yetu iwawezeshe wafanyabiashara wetu, iwape mikopo ya riba nafuu ili tutengeneze mabilionea wengine wapya. Tumechoshwa na mabilionea walewale kila mwaka.
“Tariff za kodi zinatuumiza, tuwe makini kwenye eneo hilo, tariff zetu zipo juu ukilinganisha na Wakenya, wafanyabiashara wetu wanalazimika kupandisha bei ya bidhaa lakini Wakenya wanashusha bei sababu kodi yao ni ndogo, mwisho wa siku wafanyabiashara wetu wanashindwa kuuza bidhaa zao ndani wala kupeleka nje sababu ya bei,” amesema Shigongo.
Post a Comment