Rosa Ree Avishwa Pete ya Uchumba





RAPA mkali wa kike Bongo, Rosa Ree amethibitisha kuchumbiwa na mpenzi wake, King Petrousse Rosa  amethibitisha hilo kwa kuposti video ya tukio hilo zima la kuvishwa pete hiyo jana.

 

Katika mahojiano ya usiku wa kuamkia leo na kituo kimoja cha runinga Bongo, Rosa Ree amesema kwa kifupi; “I’m ready engaged!; yaani tayari nimechumbiwa!”

 

Katika maelezo mengine ya leo asubuhi, Rosa Ree ameandika; “Nimeamka asubuhi hii kama hivi, ni kweli imetokea? Sijawahi kuota kama itakuwa hivi. Nimesema ndiyo kwa rafiki yangu mpendwa King Petrousse.”




0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post