Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi eneo la Tegeta Mkoani Dar es Salaam amesema Tozo zitaendelea kuwepo na hataki kuficha hilo
Amesema, "Tuliweka tozo kwenye mambo ya fedha za mitandao, yamepigiwa kelele sana, nimesikia. Nimekaa na Wataalamu tumepunguza 30%. Miezi miwili tuliyoanza nayo tumekusanya kama Bilioni 60 na zimepelekwa kujenga Vituo 220 vya Afya"
Ameongeza, "Januari tuna wimbi kubwa la Watoto wanataka kuingia Sekondari, lakini pia kuna wapya wanaoingia Darasa la Kwanza. Hakuna wa kutujengea ni sisi wenyewe. Fedha zitakazokusanywa Septemba na Oktoba zitaenda kujenga madarasa zaidi ya 500"
Post a Comment