"Nilijiunga na Kazi ya Ukahaba Nikiwa na Miaka 16 Licha ya Kuwa na Virusi vya Ukimwi" Regina





Katika kitengo cha ilikuaje tulikuwa naye Ragine Jane ambaye alizaliwa na virusi vya ukimwi, na kubarikiwa na kifungua mimba wake akiwa na miaka 14.

Kulingana na Regina mama yake aliaga akiwa na miaka 8 huku akilelewa na nyanya yake.

Je alipata vipi ujauzito wake wa kwanza akiwa na miaka 14
"Kwa sababu nilizaliwa na virusi vya ukimwi, tulikuwa na mafunzo ya watoto ambao wamezaliwa na virusi vya ukimwi

Nilipokuwa pale nilipatana na mwanamume ambaye nitasema alininajisi, bila ya kujali hali yangu ya afya, baada ya hapo nilipata ujauzito lakini mwanamume huyo alikuwa anajulikana sana kwa ivyo alishatakiwa


Akiwa kwenye kesi hiyo,alinambia nitoroke ili kesi iishe, nilitoroka nikaenda kuishi Mombasa lakini aliachana na majukumu yake

Mwanamume mmoja alinitambulisha kwa kazi ya ukahaba kwa maana alikuwa amechoka kunikopesha pesa, nilikuwa na miaka 16 wakati huo

Nililea mtoto wangu kwa ajili ya kazi hiyo, lakini baada ya muda nilirudi nyumbani na nikashikwa kueleza mahali nilipokuwa


Kesi iliisha ata baada ya kufanya DNA, ilhali sikupata haki yangu."

Regina alisema kwamba alibarikiwa na na mtoto wa pili,na kuweka wazi kwamba watoto wake wote hawana virusi vya ukimwi.

Alibadilika vipi au nini kilichomfanya abadilike?
"Kazi ya ukahaba haiwezi saidia mtu kwani nilifanya kwa miaka mingi lakini sikutoka na kitu chochote, wanaume wengine hawakuwa wanataka kutumia kinga wakati wa tendo la ndoa

Baada ya kesi kuisha nilipatana na mwanamume mwingine ambaye sikumwambia kwamba nina virusi vya ukimwi na nikabarikiwa na mtoto wa pili

Tuliachana na nikarudi Mombasa kufanya kazi ya ukahaba tena, kuna wakati ambapo mtoto wanggu alianguka akazirai akiwa anacheza jirani yangu aliniambia nimpeleke kanisani, baada ya mwanangu kuombewa na kuanza kutembea tena mwwaka wa 2020, nilijua kwamba kuna Mungu na napaswa kubadilika.

Nilibadilika na nikaacha kazi ya ukahaba."


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post