Mtu aliyejihami kwa bunduki awaua watu kadhaa katika chuo kikuu cha Perm




Takriban watu wanane wameuawa wakati mtu mwenye bunduki alipofyatua risasi katika chuo kikuu katika mji wa Perm nchini Urusi, maafisa wanasema.
Mshambuliaji huyo alitembea hadi chuoni humo Jumatatu asubuhi na kuanza kufyatua risasi.

Wanafunzi na walimu walijifungia ndani ya jengo la chuo kikuu; wengine walionekana wakiruka kutoka madirisha.

Haijulikani ni watu wangapi walijeruhiwa. Polisi wa Urusi wanasema kuwa mshambuliaji huyo amezuiliwa.

Kamati rasmi ya Uchunguzi ya Urusi inasema mshambuliaji huyo alikuwa mwanafunzi katika chuo hicho kikuu.

Tukio hilo lilitokea katika Chuo Kikuu cha Jimbo la Perm, kilichoko karibu kilomita 1,300 (maili 800) mashariki mwa mji mkuu, Moscow.

Video zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha wanafunzi wakirusha vitu vyao kutoka kwa madirisha kwenye majengo ya chuo kikuu kabla ya kuruka kumtoroka mshambuliaji huyo .

Sehemu hii ya video ya wanafunzi wanaoruka nje ya madirisha ilitangazwa kwenye Runinga ya Urusi:



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post