Mtoto wa Msanii wa filamu Bongo, Monalisa, Sonia ameenda kusoma Chuo Kikuu cha Summy State nchini Ukraine.
Sonia anakwenda kusomea kozi ya Uhasibu na Ukaguzi (Accounting and Auditing) kwa kipindi cha miaka minne.
"Sababu ya kuchagua kwenda kusoma nchi hiyo ni kwanza wametutangulia kiteknolojia kwa hiyo tunapoenda huko kusoma tunaweza hamisha teknolojia kwa njia ya elimu kuja hapa Tanzania"
"Kitu kingine Ukraine na Urusi ni nchi ambazo zina fursa nyingi za utalii hivyo tunavyoenda huko kusoma ni nafasi yetu kuwaambia Tanzania kuna nafasi nyingi za Uwekezaji, kuna Mlima Kilimanjaro, Tanzanite na mengine mengi ambayo Tanzania tunajivunia" amesema Sonia.
Post a Comment