Kanisa la Sinagogi, SCOAN limemteua mke wa TB Joshua, Nabii Evelyn Joshua kuwa kiongozi mpya wa kanisa hilo.
Kanisa limesema katika taarifa yake kwenye ukurasa wa Facebook kuwa programu nzima ya kanisa itakuwa chini ya uongozi wa Mungu kwa maelekezo ya Evely Joshua.
Kwa mujibu wa chapisho hilo, wakati ulikuwa sahihi, na wafuasi wa kanisa waliombwa wasali kwa ajili ya Utukufu wa Mungu.
Awali kulikuwa na tetesi kuhusu nani atakayeongoza kanisa baada ya mwanzilishi wa kanisa TB Joshua kuaga dunia mwezi Mei 2021.
Mabishano hayo yalisababisha kufukuzwa hivi karibuni kwa baadhi ya wafuasi wa TB Joshua kanisani.
Huduma ya TB Joshua ilitangaza kuwa mwanzilishi wa kanisa hilo na nabii mkuu wa Nigeria, Temitope Balogun Joshua amejiuzulu kwenye ukurasa wake wa Facebook, Jumamosi Juni 5, 2021.
Post a Comment