Lionel Messi amempiku Pele kwa kuwa mfungaji bora wa wanaume wa Amerika Kusini katika mechi za kimataifa na hat-trick katika ushindi wa Argentina katika mechi ya kufuzu kushiriki Kombe la Dunia dhidi ya Bolivia.
Kwa kufunga mabao yote katika ushindi wa 3-0 huko Buenos Aires kumefanya Messi kuwa na magoli 79 katika michezo 153.
Gwiji wa Brazil Pele alimaliza kazi yake ya kucheza soka akiwa na magoli 77 ya mechi za kimataifa kati ya michezo 92.
Bao la dakika ya 14 la Messi akiwa nje ya boksi lilimweka sawa na rekodi ya Pele kisha akavunja rekodi katika kipindi cha pili.
Mchezaji huyo wa miaka 34 alimpita mlinzi kabla ya bao lake la pili kabla ya kumaliza hat-trick dakika mbili kabla ya filimbi ya mwisho.
Baada ya mechi, nahodha wa Argentina Messi na wachezaji wenzake walisherehekea na kombe la Copa Amerika mbele ya mashabiki 20,000 kwenye Uwanja wa Monumental.
Aliongoza timu hiyo kutwaa taji hilo, taji lake kubwa la kwanza katika soka la kimataifa, mnamo Julai, akiifunga Brazil katika fainali.
"Niliitamani siku hii sana na shukrani kwa Mungu imefika," Messi aliandika kwenye ukurasa wa Instagram pamoja na picha ya timu wakiwa na kombe baada ya mechi.
"Sina maneno ya kushukuru kwa upendo wote ambao nimepata. Usiku mzuri kama nini, niliufurahia sana - usiosahaulika."
Mchezaji mwenzake anayekipiga Paris St Germain mwenye umri wa miaka 29, Neymar amefunga mabao 69 katika mechi 113 alizoichezea Brazil.
Argentina ni ya pili baada ya Brazil kwenye Jedwali la kufuzu Kombe la Dunia baada ya kushinda michezo mitano na sare michezo mitatu.
Marta anashikilia rekodi ya mabao mengi yaliyofungwa na mchezaji wa Amerika Kusini, akiwa amefunga magoli 109 kwa timu ya wanawake ya Brazil.
Post a Comment