Lowasa Edward "Samia Amerejesha nchi Kwenye Ramani"




WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowasa, amesema hotuba ya Rais Samia Suluhu, aliyotoa usiku wa kuamkia leo Septemba 24, 2021, katika Mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa amelirejesha taifa katika ramani ya dunia.

Lowasa, amesema katika kipindi kifupi alichokuwa madarakani, Rais Samia amefanikiwa kuanza kulijengea imani sekta binafsi katika kushiriki kwenye ujenzi wa uchumi.

“Safari aliyoioanzisha Rais wetu, hatuna budi sote kumuunga mkono na kumsaidia ili aliwezeshe taifa kuwa imara zaidi kiuchumi na kuiweka nchi katika utawala wa sheria.

Amesema Rais Samia, amethibitisha pasi na shaka kwamba Tanzania imepata nyota ya jaha kwa kuwa na kiongozi mkuu mwanamke hodari na shupavu ambaye leo hii tuna kila sababu ya kujivunia na kumuunga mkono.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post