Kanye West amefanya mabadiliko machache kwenye album yake "DONDA" ambayo ilitoka August 29 mwaka huu. Kanye amemuondoa kabisa Chris Brown kwenye Kolabo yao "New Again" lakini pia amefanya mabadiliko kwenye baadhi ya nyimbo kwa kufanya mixing upya kwenye wimbo kama 'JUNYA' na nyingine.
Chris Brown ni miongoni mwa wasanii ambao waliibuka na kumuangushia matusi Kanye West kwa kufuta verse zao kwenye album yake, CB alidai alishiriki kwenye ngoma mbili lakini alijikuta kwenye ngoma moja baada ya album hiyo kutoka. Sasa Kanye ameamua kumuondoa kabisa Breezy!
Post a Comment