Je, Vanessa Mdee Kajifungua Kweli au Mange Kimambi Kadanganywa Mpaka Kafuta Post?


Mara baada ya mange kimambi kupost picha ikimuonesha rotimi na mtoto mchanga na kuvujisha kwamba Ndio mtoto wao aliyezaliwa, muda si mrefu mange alisema alitafutwa na Vee na akaambiwa kuwa sio kweli wala sio mtoto wao, bali ni mtoto wa ndugu yake rotimi.

Kiukweli vanessa amemdanganya dada wa taifa, mange kimambi. Hatua aliyofikia vee inatosha kabisa kujifungua, Vee na rotimi ni wasiri sana ndio maana hata mimba imejulikana baada ya muda mrefu, je mtoto ndio atajulikana kwa muda mfupi?

Siku saba zilizopita, tayari watu walikuwa wameshaanza kukoment kwenye page ya Vee na kusema kwamba wanasikia kwa juu juu kwamba vee kajifungua, lakini vee hajawahi kureply hizo comment.

Pia siku tatu zilizopita vee amepost picha akicheza na tumbo liko wazi, mwanamke mmoja akakoment kwamba "ushajifungua wewe naona mstari kwenye kitovu umekaribia mwisho" hii ikimanisha kwamba Hiyo post ni ya zamani kabla hajajifungua.

Ukweli ni upi, Tuendelee kusikilizia mchongo, ila naamini vee ameshajifungua wiki mbili au moja nyuma, ila daaah vee bana msiri sana, madada zetu wa buza wangetangaza mapema sana.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post