Hata Nje za Nchi Maisha ni Magumu..Formula ni ile ile Duniani Kote


Dhana ya mafanikio ughaibuni ni dhana nzuri sana na inavutia na kusisimua kwa kila anaeisikia. Kwasababu ya picha tunazoziona kwenye smartphone zetu namna ya mafanikio yalivyo kwa wenzetu.

Lakini ni hatari sana kwenda nje ukiwa bado akili yako haijangundua uhalisia wa sehemu unayotaka kwenda na utaenda kufanya nini. Nivyema tukapigana msasa kwenye vichwa vyetu kwa kuelezana mambo yenye kujenga kuhusu kesho yetu.

Kuna watu wamepoteza heshima zao na hadhi zao kwasababu ya sauti ndogo inayosikika kwenye masikio yao kuwa ughaibuni maisha mepesi. Hii ni dhana tamu sana yenyekuvutia kila mtu mwenye kiu ya mafanikio. Ila lazima ujue unachotaka kwenda kufanya huko unapotaraji kwenda.

Hakuna hata sehemu moja katika hii dunia ambayo maisha yatakuwa mazuri kwa kukaa kijiweni unapiga soga na marafiki. Fomula ya mafanikio ni ile ile popote utakapokwenda kuishi lazima uifate.

Lazima ujitume na ufanye kazi kwa ufanisi bila kukata tamaa hicho ndio kitu pekee kitakacho kufanya ufanikiwe popote utakapokuwa katika hii dunia. Hakuna hata nchi moja ambayo utakuta hela zinamwaga chini ukazipata kwa wepesi.

Tuliza akili yako vizuri brother kama akili yako haijapevuka vyema bora utulie nyumbani ule ugali wako na uduvi usitake kwenda kusumbua watu kwasababu ya uvivu wako. Maisha ni magumu kila sehemu kama huna nidhamu ya maisha take care.

Na: @abdulrazaki.issa


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post