Harmonize Matatani Tena Kupita na Mistari ya Dully Kwenye Nyimbo yake Mpya...Dully Afunguka

Reposted from @sajomedia DULLY ABAINISHA ISHU YA HAKI MILIKI DHIDI YA HARMONIZE.


Kwenye wimbo wa @harmonize_tz unaoitwa Teacher, kuna baadhi ya mistari ambayo ameichukua kutoka kwenye wimbo wa msanii Dully Sykes unaoitwa Bongo Flava. Hasa Dully amebainisha kuwa suala hilo lipo mikononi mwa wanasheria wake na ameambiwa hasilitolee ufafanuzi zaidi.

Uwenda tunaweza shuhudia Dully akimchapa faini konde boy kwa madai ya Haki miliki na inaonyesha hadi suala hili kufika mikononi mwa wanasheria ni wazi hakukuwa na makubaliano yoyote kati yao.

Japo Dully amethibitisha kuwa hana tofauti na msanii yeyote yule na anaweza fanya kazi na Harmonize lakini alichokiongea kina uwalakini na ukizingatia toka Harmonize atoke WCB ndipo ukaribu wake na Dully Sykes ukapungua.




0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post