Gerson Msigwa Ashindwa Kujizuia Baada ya Mtangazaji Lily Ommy Kufanya Interview na Rick Ross, Afunguka Haya



Umefanya jambo kubwa sana kwa Tanzania. Haya ndio mambo natamani sisi Wanahabari tujivunie.

Tutambe kwa kalamu zetu kujenga nchi, kuitangaza nchi, kuitetea nchi, kuwapigania Watanzania, kuvutia wawekezaji na biashara ili Watanzania wenzetu wanufaike kwa ajira, pesa, maisha mazuri, michongo ya kimataifa, connections kubwa na mengine mengi.

Haiwezi kuwa sifa kama kalamu zetu tutatumia kuleta tafrani, taharuki, uchonganishi, kuua uchumi, kutisha wawekezaji, kuvuruga biashara na kupigia debe ajenda za mataifa mengine yanayotafuta kujinufaisha kutoka kwetu.

Nimesema na narudia, kabla ya kuandika jambo lenye madhara kwa Tanzania tujitafakari kama ni sawa kuiharibu Tanzania ambayo Watanzania wenzetu wameijenga kwa jasho jingi na damu tangu Uhuru?

Nawapongeza Waandishi wa Habari wenzangu wote tunaofanya wajibu huu vizuri, tusichukulie poa na tutembee kifua mbele.

Leo @richforever akija kuwekeza Tanzania Watanzania wenzetu wangapi watanufaika? Ataitangaza Tanzania kwa mamilioni ya watu duniani wakiwemo Watalii.

Again bigup @lilommy this stuff is fantastic. Umeupiga mwingi sana mdogo wangu, keep it burning Bro.

Pia shukrani kwa my Dada @hamisamobetto umetufaa kinomanoma. Hili ni bonge la connection. Endelea hivyo hivyo.
#KaziIendelee


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post