Dizaini kama Battle kati WCB na KONDE GANG limekuja na sura nyingine. Ukiachilia mbali wasanii kurushiana vijembe kwenye nyimbo zao,lakini pia Machawa waka wameingilia kati kutetea maboss wao.
Roundi hii pia vita imegeukia kwa wapiga picha wa mastaa hawa wa pande zote mbili. Alianza @jabulant_ ,Videographer wa @harmonize_tz ambae aliweka Insta Story yake akidai kama hauko Marekani basi wewe sio msanii mkubwa ama videographer mkubwa maana wasanii wakubwa na mavideographer wakubwa wapo kwa mjomba Biden😁
@lukambaofficial akaona isiwe kesi ngoja amjibu,akajibu pia kwa Insta story lakini ameona haitoshi kaja kujibu pigo kwenye wall yake kabisa akiandika kwa kuuliza ni Marekani gani ambayo wapo, maana hata promoter wao hamuoni huku akiambatanisha post hiyo na picha ambayo amepiga na Wiz Khalifa😁.
Post a Comment