DC Msando atangaza kukatwa Mshahara, ataja sababu




Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Albert Msando amesema anakatwa Milioni 2 na laki nane kati ya milioni tatu na laki moja kutoka kwenye Mshahara wake kama rejesho baada ya kukopa kiasi cha Shilingi milioni 106 katika moja ya taasisi ya Fedha ili kutengeneza vibanda vya Machinga.

“Mheshimiwa Rais aliona mimi inmpendeza kuniteua kuwa Mkuu wa Wilaya na mimi kama Mkuu wa Wilaya nikaona nikope benki kwa kutumia mshahara wangu wote kwa muda nitakaotumikia”- DC Msando
 
“Wakanipa Shilingi Milioni 106 nimekopa kwa niaba ya Machinga na katika pesa hiyo niliyoikopa na ndio nimekuja  kumalizia mabanda haya ya wamachinga, imani yangu ni kwamba Machinga lazima tumnyajue”- DC Msando



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post