Christian Bella "Sio Lazima Ulambe Lips Ndio Utrendi"



Zee la Masauti na Founder wa Malaika Band, @bellachristian1 Obama ametoa Darasa kwa wasanii wengine kutumia majina yao vizuri, kuyatumia nje ya kile wanachokifanya ikiwemo uwekezaji nje ya muziki maana kuna leo na kesho, kitu ambacho yeye alikifanya wakati anapata jina na haijawahi msumbua hata hasipofanya show.

Mkali huyo wa Melody aliyeanza kutamba na hits kibao hata kabla ya mapinduzi ya Social Networks ikiwemo "Yako wapi Mapenzi, mwaka 2006" amedai anaweza hasiwepo kwenye trending lakini akawa anafanya poa sawa na wale wanaotrend kwa wakati huo huku akidai kutrend sio lazima ujilambe lips au kujipost post bali kufanya muziki mzuri ambao hata kesho utaishi na watu wataupenda.

Bella kwa sasa amekuja na vijana, @cbomusic_ mbali na Malaika Band ambao anadai kwa asilimia kubwa amewapata wakati yeye ni Judge kwenye mashindano ya BSS msimu uliopita na akaona wana kitu ndani yao na kwasasa wameachia dude linaitwa MARIANA. Pita kwenye Account yao utakutana Bio pale then ishi uenjoy Melody🔥


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post